
Wahusika wa vyombo vya usafirishaji majini mna mengi sana ya kuiambia Dunia na sisi Watanzania kuh hili janga kwani yale maumivu ya Mv Bukoba yameturudia tena(Waswahili wa pwani wanasema nimekusamehe lakini sitokusahau)
Leo neno liko ndani ya vinywa vyetu japo tulishukuru kwa yaliotokea lakini machungu yamerudi tena kwa kuwapoteza ndugu na jamaa zetu,...Msipange nauli tuu au kuchukua kodi za ushuru wa vyombo tuvitumiavyo mna majukumu mengine ya kuangalia.

Sakina H Jalala ni mtoto wa kaka yangu mkubwa siku chache toa afunge ndoa na mume wake walikuwa akisafiri toka kwenye mji wa Bagamoyo kuelekea Zanzibar kwa boti chombo chao kilikumbwa na dhoruba na kuzama kwa kuwa alikuwa hajui kuogelea alitapatapa sana kwenye maji na ikabidi mume wake afanye kazi ya ziada kuogelea nae na kushikilia kipande cha ubao.Alikunywa maji mengi sana na kupoteza fahamu alipozinduka akajikuta yuko hospitalini kwa kuokolewa na wavuvi siku ya pili yake akiwa peke yake na maiti ya mume wake iliokotwa kwenye kijiji cha Mlingotini na habari zilitufikia siku tatu baada ya tukio,
INNA LILLAH WAINNA ILAAH RAJIUN
Kwa huzuni na majonzi makubwa
Na http://mpituli.blogspot.com