Monday, 12 September 2011

AJALI YA MELI MENGI YENYE SIMANZI KUJULIKANA

Hivi ndio mambo yanavyokuwa pindi tunaposafiri toka au kuelekea visiwani,Kwenye kila nyumba tatu ya nne tano yake kuna msiba ikiwa Mama kampoteza mwanae au mumewe basi hali kwa wengine ni Baba kampoteza mke wake na hata watoto,Watoto nao aidha wako peke yao Baba na Mama wote wamefariki,Kinacho umiza kichwa kuna watoto waliobakia peke yao Wazazi ndugu wote wamefariki INNA LILLAH WAINNA ILAAH RAJIUN,
Wahusika wa vyombo vya usafirishaji majini mna mengi sana ya kuiambia Dunia na sisi Watanzania kuh hili janga kwani yale maumivu ya Mv Bukoba yameturudia tena(Waswahili wa pwani wanasema nimekusamehe lakini sitokusahau)
Leo neno liko ndani ya vinywa vyetu japo tulishukuru kwa yaliotokea lakini machungu yamerudi tena kwa kuwapoteza ndugu na jamaa zetu,...Msipange nauli tuu au kuchukua kodi za ushuru wa vyombo tuvitumiavyo mna majukumu mengine ya kuangalia.
Kama kuakikisha hivi vyombo vina vitu vya kuokolea maisha yetu pale ajali inapotokea.Ikiwa chombo cha usafiri majini kina uwezo wa kubeba abiria 500 basi lazima kuwe na maboya ya kuokolea 550 yaani hamsini zaidi:Hii inajulikana hata kama ujui sheria kwani si mnajua MFA MAJI HAISHI KUTAPATAPA;Kifo ni kifo lakini cha maji kigumu sana kama uliwai kuzama majini na ukanusulika kufa hakika utajua nini naongelea Wahusika tunawaomba muwe makini na kazi zenu...


Sakina H Jalala ni mtoto wa kaka yangu mkubwa siku chache toa afunge ndoa na mume wake walikuwa akisafiri toka kwenye mji wa Bagamoyo kuelekea Zanzibar kwa boti chombo chao kilikumbwa na dhoruba na kuzama kwa kuwa alikuwa hajui kuogelea alitapatapa sana kwenye maji na ikabidi mume wake afanye kazi ya ziada kuogelea nae na kushikilia kipande cha ubao.Alikunywa maji mengi sana na kupoteza fahamu alipozinduka akajikuta yuko hospitalini  kwa kuokolewa na wavuvi siku ya pili yake akiwa peke yake na maiti ya mume wake iliokotwa kwenye kijiji cha Mlingotini na habari zilitufikia siku  tatu baada ya tukio, 
INNA LILLAH WAINNA ILAAH RAJIUN
Kwa huzuni na majonzi makubwa 
Na http://mpituli.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Angalia unapoandika usije kuleta machafuko
na hali ya sinto fahamu