Friday 30 December 2011

KIDUME CHAACHA KULIPULIZA



Ardi Rizal, 2, fick en första cigarett av sin pappa när han var 18 månader.Alianza kupuliza swaaaleti akiwa na wiki
 kumi na nane na upadrii au na ushee hivi na kufikia kuvuta fegi 40 kwa siku sio mwengine ni yule yule dogo mpulizaji Tema.sasa aacha kuvuta swahaleti fegi
isiokuwa na nongwa kwa vyombo vya serikali na vyenginevyo.kwa jitihada za mama yake ya kupambana na mpulizo atimae amefanikiwa kumkomboa mwanae kwa maradhi yatokanayo na moshi karibu na Atown..

Wednesday 14 December 2011

JUA TOKA NIANIKE KIBANGILE CHANGU

Leo mitaa ya Stochnyoko kijua kimewaka kimtindo na hata hapa Ottaya Oslo mambo si mabaya kwa swana

Monday 5 December 2011

ALIKUWA RAIS AKAWA WAZIRI MKUU SASA RAIS TENA


Si mwengine bali V Putin.Baada ya uchaguzi ameibuka kuwa mshindi na chama chake kurudi tena Ikulu baada ya kushindwa kwenye uchaguzi uliopita na kumuwezesha rais aliepita kumchagua kuwa waziri mkuu.Gazeti moja maarufu la kila siku limedadavua ya kuwa Putini bado ni kipenzi cha wa Rusia na kiongozi mwenye kujua kazi yake ipasavyo KILA LA KHERI PUTIN

Wednesday 30 November 2011

NA HII NI MEXICO


UKANDA NASI ULIOBORA PICHA NA MUASISI WETU MEXICOcid:DFF337368AE0469987F2CBB68A569DF9@MWANJELWA010

Monday 12 September 2011

AJALI YA MELI MENGI YENYE SIMANZI KUJULIKANA

Hivi ndio mambo yanavyokuwa pindi tunaposafiri toka au kuelekea visiwani,Kwenye kila nyumba tatu ya nne tano yake kuna msiba ikiwa Mama kampoteza mwanae au mumewe basi hali kwa wengine ni Baba kampoteza mke wake na hata watoto,Watoto nao aidha wako peke yao Baba na Mama wote wamefariki,Kinacho umiza kichwa kuna watoto waliobakia peke yao Wazazi ndugu wote wamefariki INNA LILLAH WAINNA ILAAH RAJIUN,
Wahusika wa vyombo vya usafirishaji majini mna mengi sana ya kuiambia Dunia na sisi Watanzania kuh hili janga kwani yale maumivu ya Mv Bukoba yameturudia tena(Waswahili wa pwani wanasema nimekusamehe lakini sitokusahau)
Leo neno liko ndani ya vinywa vyetu japo tulishukuru kwa yaliotokea lakini machungu yamerudi tena kwa kuwapoteza ndugu na jamaa zetu,...Msipange nauli tuu au kuchukua kodi za ushuru wa vyombo tuvitumiavyo mna majukumu mengine ya kuangalia.
Kama kuakikisha hivi vyombo vina vitu vya kuokolea maisha yetu pale ajali inapotokea.Ikiwa chombo cha usafiri majini kina uwezo wa kubeba abiria 500 basi lazima kuwe na maboya ya kuokolea 550 yaani hamsini zaidi:Hii inajulikana hata kama ujui sheria kwani si mnajua MFA MAJI HAISHI KUTAPATAPA;Kifo ni kifo lakini cha maji kigumu sana kama uliwai kuzama majini na ukanusulika kufa hakika utajua nini naongelea Wahusika tunawaomba muwe makini na kazi zenu...


Sakina H Jalala ni mtoto wa kaka yangu mkubwa siku chache toa afunge ndoa na mume wake walikuwa akisafiri toka kwenye mji wa Bagamoyo kuelekea Zanzibar kwa boti chombo chao kilikumbwa na dhoruba na kuzama kwa kuwa alikuwa hajui kuogelea alitapatapa sana kwenye maji na ikabidi mume wake afanye kazi ya ziada kuogelea nae na kushikilia kipande cha ubao.Alikunywa maji mengi sana na kupoteza fahamu alipozinduka akajikuta yuko hospitalini  kwa kuokolewa na wavuvi siku ya pili yake akiwa peke yake na maiti ya mume wake iliokotwa kwenye kijiji cha Mlingotini na habari zilitufikia siku  tatu baada ya tukio, 
INNA LILLAH WAINNA ILAAH RAJIUN
Kwa huzuni na majonzi makubwa 
Na http://mpituli.blogspot.com