Sunday 28 October 2012

NATAKA KULEWA (NEW TRACK OF DIAMOND)

Kitu kipya cha Dimond kitakacho kwenda kwa jina NATAKA KULEWA kitakuwa hewani hivi punde

IDD MUBARAQ

Sisi wa Mpituli tunawatakia waislam wote duniani sikukuu njema ya idd na kheri zake

Monday 15 October 2012

Alhaji Mintanga sasa huru

Ni baada ya kukaa mahabusu kwa zaidi ya miaka minne akituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya


Saturday 6 October 2012

HAPPY BIRTHDAY MRISHO JAKAYA KIKWETE

LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA RAIS WA JAMHURI WA TANZANIA MH KIKWETE,SISI WA MPITULI TUNA MTAKAIA MAISHA MAREFU  YENYE FURAHA
UZIMA NA AMAN KWAKE NA FAMILA YAKE 


JK ZIARANI NCHINI CANADA

Kikazi zaidi
 

WIKI END HII PEMBEZONI MWA BAHARI

Msomaji wetu katuletea hili tangazo hapo ndani ya TASUBA chuo cha sanaa pembezoni kabisa mwa bahari kutawaka moto


Wednesday 19 September 2012

HALI YA HEWA IMEANZAA KUBADILIKA

Majira ya baridi ndio hayo kwa wanaoishu pande zile za kule muda ndio huu wa kulisogeza koti

Tuesday 18 September 2012

BWAGAMOYO YAZIDI KUNG ALA



JK Aweka Jiwe La Msingi uzinduzi  Ujenzi Wa Barabara Ya Bagamoyo-Msata


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Msata uliofanyika katika kijiji cha Kiwangwa wilayani Bagamoyo leo mchana.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi, Kaimu Mkuu wa mkoa wa Pwani ambaye pia ni mkuu  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik(Wapili kushoto),Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli(wanne kushoto) na kulia ni Waziri wa Mazingira Mhe. Theresa Hoviza.

Ndoto ya miaka mingi ya kujengwa kwa barabara ya Msata-Bagamoyo kwa kiwango cha lami imetimia leo, Jumanne, Septemba 18, 2012, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipoweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara hiyo katika sherehe kubwa iliyofanyika eneo la Kiwangwa.
Barabara hiyo ya kilomita 64 inajengwa na mkandarasi wa ndani ya nchi, Estim Construction, na inagharimiwa asilimia mia na Serikali ya Tanzania bila msaada kutoka kwa mfadhili yoyote.Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania, Injinia Patrick L. Mfugale amesema kuwa barabara hiyo inayogharimu kiasi cha Sh. bilioni 94, ikiwa ni pamoja na fedha za fidia na kumlipa mkandarasi mshauri, itakamilika Juni mwakani.

Pamoja na kwamba Mheshimiwa Rais ameweka jiwe la msingi kwenye barabara hiyo, Injinia Mfugale amesema kuwa mkandarasi wa sasa alianza ujenzi tokea 2010 baada ya usanifu wa barabara hiyo kukamilika na baada ya Serikali kumtimua mkandarasi wa mwanzo wa barabara hiyo, TACOPA, Novemba 13, mwaka 2009.Amesema kuwa mpaka sasa barabara hiyo imekamilika kwa asilimia 65, yaani kwamba kiasi cha kilomita 36.7 tayari zimewekwa lami na kuwa ni kilomita 23 zilizosalia na ambazo zitamalizika katika miezi tisa ijayo.Injinia Mfugale amesema kuwa mpaka sasa Serikali imekwishakulipa kiasi cha Sh. bilioni 56.8 ikiwa ni pamoja na fedha iliyolipwa kama fidia kwa wananchi ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo.Amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo hautahusisha ujenzi wa daraja kwenye Mto Ruvu kwa sababu usanifu wa daraja hilo ulichelewa kidogo kukamilika hata kama tayari sasa umekamilishwa.

Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa John P. Magufuli amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ni sehemu ya ujenzi wa kilomita 11,154 za barabara za lami zinazojengwa na Serikali ya Mheshimiwa Kikwete.“Nataka muelewe vizuri maana ya kilomita hizi. Wakati wa Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, tulikuwa na barabara za lami zenye urefu wa kilomita 1,330. Kati ya Uhuru na mwaka 2005, tulijenga barabara zenye urefu wa kilomita 6,500 na kati ya 2005 na sasa tunajenga barabara zenye urefu wa kilomita 11,154,” amesema Waziri Magufuli.Waziri huyo amerudia msimamo wake kuwa kamwe Serikali haitawaachia watu wanaojenga ama kufanya shughuli katika eneo la hifadhi ya barabara bila kuwachukulia hatua.

Naye Rais Kikwete amewaambia mamia kwa mamia ya wananchi walioshiriki katika sherehe hizo kuwa barabara ndiyo mishipa ya damu ya uchumi wa nchi yoyote na ndiyo maana Serikali inatenga kiasi kikubwa katika Bajeti yake kwa ajili ya ujenzi wa barabara. Amesema kuwa katika Bajeti ya sasa, barabara zimetengewa kiasi cha Sh. trilioni 2.2 ambacho ni kiasi kikubwa cha pili baada ya Bajeti ya elimu.Rais Kikwete amesema kuwa pamoja na faida zake kubwa na nyingi, barabara hiyo itakuwa na changamoto zake ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ajali za barabara, kuongeza urahisi wa kusambaa kwa ugonjwa wa ukimwi na hata kuvutia watu wenye lengo la kununua ardhi kubwa ya wanavijiji ambako inapita barabara hiyo.Rais pia ameungana na Waziri Magufuli kwa kuonya: “Kama alivyosema Waziri, wanaoifuata barabara watavunjiwa nyumba zao na hawatalipwa, lakini wale ambao barabara inawafuata watalipwa hata wakivunjiwa.”

Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu.Dar es Salaam. 18 Septemba, 2012

Thursday 13 September 2012

Amuacha aliemsachi kwenye reli

Mannen lämnar perrongen - efter att ha rånat Jerry som ramlat ner på tunnelbanespåret.
Mtu anaetafutwa kwa udi na uvumba nchini sweden baada ya kumsachi na kuondoka na poketi uku traini kuja na kumkanyaga jamaa anaefahamika kwa jina la Jerry


Monday 10 September 2012

STAZ 2 GAMBIA 1 NA GOZI Limekwisha


Mpira umekwisha na Tanzania 2 Gambia 1

Serena Williams ashinda US open

Tre stora tennistitlar på lika många månader är inte nog. Efter US Open-segern är Serena Williams fortfarande hungrig på fler titlar.

Ajisikia kijana mwenye njaa kwa ushindi wake,ameshinda Victoria Azarenka6-2,2-6,7-7

Thursday 6 September 2012

UJENZI BAGAMOYO ROAD UNAVYOENDELEA

Ujenzi wa barabara ya Bagamoyo unazidi kusonga mbele na wenye matumaini makubwa licha ya foleni za hapa na pale lakini mambo mswano

ONYO PICHA HIZI ZA KUTISHA


TUKIO LA KUUWAWA DAUDI MWANGOSI AKIWA MIKONONI MWA WALINDA AMANI 2012 MJINI IRINGA


Picha hii ni kwa hisani ya mtandao.Bint akimuangalia baba yake Sheakh Aboud Rogo muhubiri wa dini ya kiislam mjini Mombasa Kenya aliepigwa risasi hivi karibuni haya ndio yaliojili Afrika mashariki...Tunaomba viongozi wetu kukemea haya mambo kwa nguvu zao zote

Tuesday 4 September 2012

MICHAEL DUNCAN TUTAKUKUMBUKA

Michael Clarke Duncan in The Green Mile
Galasa maarufu la cinema Michael Clarke mwana wa Duncan amefariki dunia baada ya 

kuugua kwa muda miezi mitatu kitandani kwa kusumbuliwa na ugonjwa wa 

moyo.Amekufa jijini Los Angeles siku ya jtatu 

Hakika mashabiki wake watamkumbuka kwa umahili wake wa kucheza cinema

AFRICA HAKUNA NJIA YA MKATO UKUAJI WA MIJI NA MAKAZI

Umoja wa Mataifa umeweka bayana kuwa hakuna njia ya mkato ya kukabilina na changamoto za kukuwa kwa miji zaidi ya kuwa na sera madhubuti za kuboresha na kupanua miji. Mwanzoni mwa karne ya 20 ni 2% tu ya watu ilikuwa ikiishi mijini. Leo ni 50%.

Picha pembeni ni jiji la Dar es salaam kama ilivyo naswa na ngwamba letu

Zetu dua unyonge una mwisho wake


KURA YA MAONI

Ni halali Polisi kutumia nguvu kupita kiasi?


 
 
 
 

Lango la dhahabu lenye ulinzi wa chuma

Lango kuu la dhahabu kwenye bustan mwanana yenye mandhali kuvutia ndani ya himaya malkia Victoria wa Scundanavia

ETI TUME YA NINI NA WAHUSIKA HAWA HAPA?


Mambo haya mpaka lini?mbona orodha inazidi kuongezeka,Songea.Arusha.Morogolo.Iringa na kwengineko 

Leo tuko shamba

Kwa mapicha na manyuzi ya shambazz yatakuwepo kama dawa kama kawa

Tuesday 24 July 2012

WAZO LA MDAU KWA MH SPIKA MAKANDA


Mdau anafunguka hivi ikiwa kama utoro unashamil Bungeni hadi kupelekea kukamishwa kwa bajeti  kwa nini Spika asiwe anaita majina kabla ya kuanza kikao cha bunge na asie kuwepo aulizwe sababu zilizo mfanya asiwepo bungeni kama hazikuwa na umuhimu kwa taifa achapwe viboko kama kwenye shule za msingi enzi zile.Kwani kitendo cha kusaini uwenda kukawa na kajimchemzo fulani kisicho faa 

Friday 20 July 2012

KWA NINI KILA KUKICHA NI SISI TUU

Wakati ndio huu inabidi tujifunze kutokana na makosa...Meli ilifungiwa toka mwaka 2009 kusafirisha abiria sisi tukaenda kuinunu na kuanza kusafirisha abiria...
Vyombo vyetu vya usalama tuvisikia vikidai ilikuwa imechikiwa na haikuwa na tatizo kwa maana haikuwa na dosali ikaanza kazi na matokeo yake imeshindwa kumudu dharuba ya dakika kumi na kusabisha maelfu kufariki dunia.....Hivi lini sisi tutakaa chini na kuanza kusoma alama za nyakati?
NI WAKATI WA KUJIFUNZA KUTOKA NA MAKOSA 

JK NDANIYA YAUMUL IJUMAA HII LEO


JK akiwa na Makamu wake Dr Bilal pamoja na  waislam  (Zanzibar ) kwenye swala ya ijumaa
Picha mdau white house Tza

Thursday 19 July 2012

MSAFIRI KAKILI

Wengi tunasema msafiri katili wengine wanasema msafiri kafili
yote ni misemo ya wahenga waliotangulia
Mdau akiwa safarini kuvuka bahari kuelekea anakoelekea

MSIBA UGONGAO MOYO TANZANIA VISIWANI

TAARIFA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA
LA MAPINDUZI, MHESHIMIWA DK. ALI MOHAMED SHEIN,
KUHUSU AJALI YA MELI YA MV SKAGIT YA KAMPUNI YA SEAGUL
JULAI 18, 2012

                                                                                      BISMILLAH RAHMAN RAHIM
Ndugu Wananchi
,
ASSALAMU ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH
Kwa masikitiko makubwa leo Jumatano, Julai 18, 2012 nchi yetu imepata tukio la huzuni kubwa la ajali ya kuzama meli ya mizigo na abiria ya MV SKAGIT tukio ambalo limesababisha vifo, majeruhi na kupotea mali za watu.
Ajali hiyo imetokea wakati meli hiyo ilikuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuja Zanzibar. Taarifa za awali za MV SKAGIT ni kuwa meli hio ilikuwa na jumla ya watu 290. Kati ya hao wafanyakazi ni watu 9, abiria watu wazima ni 250 na watoto 31. Meli hiyo ilipata maafa hayo maeneo ya Kisiwa cha Chumbe milango ya saa nane mchana. Mara baada ya taarifa ya ajali hiyo kutufikia, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikishirikiana na taasisi mbali mbali zikiwemo Idara Maalum za SMZ, Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mamlaka ya Usafiri wa Baharini pamoja na vyombo vya usafiri wa baharini vya watu binafsi na wananchi kwa jumla ilichukua hatua za haraka kufika eneo hilo kwa kazi za uokozi.
Mpaka saa za magharibi hivi leo, idadi ya watu waliookolewa 136 na maiti 31 wamepatikana, wakiwemo watu wazima 24 akiwemo raia wa kigeni mmoja na watoto 7. Jumla ya watu 123 bado hawajaonekana. Juhudi za uokozi ziliendelea hadi kuingia giza na zitaendelea mara kukipambuzuka. Hali ya bahari ilikuwa mbaya wakati huo na meli hiyo ilipinduka katika mawimbi makubwa.
Ndugu Wananchi,
Tukio hili ni msiba mkubwa kwa wananchi wote wa Zanzibar na taifa la Tanzania kwa jumla. Ni wakati mgumu kwetu sote na napenda kutoa wito kwa watu wote tuwe na subira na wastahamilivu. Huu ni wakati wa kufikiria ndugu na watoto wetu waliopoteza maisha yao na tuwatakie rehema za Mola wetu. Aidha, tunawaombee nafuu waliopata majeraha.
Kwa niaba yangu binafsi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar natoa pole kwa wafiwa wote na namuomba Mwenyezi Mungu awape subira. Kwa wale ambao bado hawajapata taarifa za watu wao waliokuwa katika safari hiyo, nawaomba wawe wavumilivu wakati tunafanya juhudi zote za uokozi na utafutaji miili ya waliofariki.
Vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi mbali mbali vitaendelea kuchukua kila hatua inayofaa katika kazi hiyo. Natoa shukurani zangu na za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa wenye vyombo vya bahari binafsi vilivyoshiriki katika kazi za uokozi na kuokota maiti na pia wananchi wengine waliojitolea. Kadhalika, navishukuru vyombo vya habari kwa kuendelea kuwaarifu wananchi tukio hili kila hatua. Ni matumaini yetu kwamba wataendelea kushirikiana na sisi katika kushughulikia tokeo hili.
Ndugu Wananchi,
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itasimamia gharama zote za mazishi ya wale waliofariki na pia itatoa huduma ya afya, matibabu na nyengine kwa wote waliopata majeraha. Tutatangaza mipango yote kupitia vyombo vya habari na njia nyengine.
Kutokana na msiba huu, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatangaza siku tatu za maombolezi kuanzia kesho tarehe 19 Julai, 2012. Katika kipindi hicho sherehe na tafrija zote zinazatakiwa kusitishwa. Bendera zote zitapepea nusu mlingoti.
Nawasihi wananchi kuwa huu si wakati wa kutupiana lawama au kueneza habari zisizothibitishwa. Sote tushirikiane na kusimama pamoja katika tukio hili la msiba na maafa. Tukubali kuwa msiba huu ni amri ya Mwenyezi Mungu na umeandikwa kuwa mtihani kwetu. Mola wetu anatuambia kuwa binadamu tutapewa mitihani ya kupoteza maisha na mali. Huu ni mtihani mmojawapo wa hiyo. Tumuombe Mwenyezi Mungu atupe subira.
Ina Lillahi Waina Ilayhi Rajiiun.

Wednesday 18 July 2012

MELI YAZAMA KARIBU NA KISIWA CHA CHUMBE

Yenye idadi ya abiria 380 juhudi za kuwaokoa zinaendelea..Picha toka maktaba yetu

Sunday 15 July 2012

Saturday 14 July 2012

KIMAWASILIANO ZAIDI

Billiga telefonerZOTE ZIKO HEWANI..UKIJIHSANGAA UTASHANGALIWA

Afande lindoni

Mitaa ya jiji la Stocholm kwenye jumba la mfamle.Picha na ngwamba letu

Wednesday 11 July 2012

WAHENGA WANASEMA:NAZI HAIWEZI KUSHINDANA NA JIWE


Taarifa Kwa Umma

Baraza la Madaktari Tanganyika limepokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwamba, baadhi ya Madaktari waliopata usajili wa muda ili kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo (Internship), waligoma kutoa huduma kwa wagonjwa kati ya tarehe 23 na 29 mwezi Juni 2012. Madaktari hao walipangiwa kutoa huduma kwa wagonjwa katika hospitali za Muhimbili, K.C.M.C, Rufaa Mbeya, Bugando, Amana, Temeke,St. Francis- Ifakara, Mwananyamala, Sekou Toure, Haydom na Dodoma. Kufuatia mgomo huo, uongozi wa hospitali husika uliwaandikia barua iliyomtaka kila daktari aliyeshiriki kwenye mgomo kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii aliwasilisha malalamiko kwenye Baraza la Madaktari Tanganyika kwamba, Madaktari waliogoma walikataa kutoa huduma za kitaalamu, ikiwa ni wajibu wao, na kwamba kitendo hicho kilihatarisha maisha ya wagonjwa katika hospitali husika na pia ni kinyume na maadili ya taaluma ya udaktari. 
Kufuatia malalamiko hayo, Msajili wa Baraza la Madaktari Tanganyika, alimwandikia kila daktari aliyelalamikiwa Taarifa ya Kusudio la Kufanya Uchunguzi (Preliminary Examination) dhidi yake, juu ya malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Baraza la Madaktari Tanganyika limebaini kuwa, kwa mujibu wa kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Madaktari, Sura ya 152, Madaktari waliokuwa kwenye mgomo na ambao kwa sasa wameondolewa katika hospitali walizokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo, wamepoteza sifa za kupata usajili wa muda (Provisional Registration).
Kwa kuzingatia masharti ya Sheria kuhusu kupata usajili wa muda, Baraza la Madaktari Tanganyika limeridhika kwamba madaktari wote ambao majina yao yameorodheshwa katika Taarifa hii, wamepoteza sifa na kwa sababu hiyo, usajili wao umesitishwa kuanzia tarehe 11 Julai, 2012. Madaktari wote wanaohusika wanatakiwa kurejesha hati za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari kabla ya tarehe 17 Julai, 2012.
S/NO JINA REG. NO. 
MUHIMBILI 
1 Dr. Dickson N. Sahini 363
2 Dr. Elphas G. Mrita 4902
3 Dr. Anastazia E. Komba 4973
4 Dr. Anna Lwemunge 5086
5 Dr. Mariam Amour 4974
6 Dr. Jackline Matowo 5372
7 Dr. Baya Kisiwa 4970
8 Dr. Lilian B. Komba 4871
9 Dr. Pavina Kazaura 5089
10 Dr. Herifrid Kimambo 5377
11 Dr. Kokuhabwa Mukurasi 5095
12 Dr. Evance Godfrey 5059
13 Dr. Emmanuel K. Luchagula 4874
14 Dr. Florence Mtei 5094
15 Dr. Alfonse Moyo 5097
16 Dr. Alkwinus Kabwogi 4889
17 Dr. Rebeca A. Kalikawe 4962
18 Dr. Aida O. Salum 5368
19 Dr. Aron Aron 5345
20 Dr. Sabza Masoud 4956
21 Dr. Ramadhani Kabota 4861
22 Dr. Norbert Benjamin 
23 Dr. Victroia Paul 5084
24 Dr. Godfery Chuwa 5097
25 Dr. Goodluck Mrosso 356
26 Dr. Luciana Albert 375
27 Dr. Gendagenda Mkombozi 372
28 Dr. Lucas Mselle 4919
29 Dr. Edna Mwakyembe 365
30 Dr. Haruna Rashid 552
31 Dr. Sara Lumumanji 5006
32 Dr. Paul Zacharia 4858
33 Dr. Abza Saka 4981
34 Dr. Baraka Maige 5361
35 Dr. Wilhelmuss I. Mauka 4979
36 Dr. Deogratius Mally 4960
37 Dr. Ahmad Fadhil Kombo 4868
38 Dr. Iman Bawazir 4799
39 Dr. Frank Kagoro 5046
40 Dr. Baraka Yessaya 5058
41 Dr. Naki Kiroga 5347
42 Dr. Bakari A. Gillal 4959
43 Dr. Linda August 5343
44 Dr. Shah Alkash 342
45 Dr. Chihoma Mhaki 358
46 Dr. Gloria Leo 337
47 Dr. Mohamed M. Ally 
48 Dr. Ahmed Kombo 5389
49 Dr. Steven Nandi 5030
50 Dr. Moses J. Karashani 5040
51 Dr. Innocent Mpuya 5371
52 Dr. Octar Javett 5048
53 Dr. Juma Mbugi 5018
54 Dr. Neema Nalitolela 4966
55 Dr. John Nkenda 4963
56 Dr. Ngutuni Jackson 5005
57 Dr. Malava F. Raphael 4982
58 Dr. Masawa Nyamunjeku 5000
59 Dr. Shubi Matovelo 4976
60 Dr. Winnie Temu 4965
61 Dr. Sarah Shiraz 5024
62 Dr. Hafsa Hawesi 5369
63 Dr. Anthony Kingilo 5330
64 Dr. Elikanaar Urio 5336
65 Dr. Zainabu Mkinde 5367
66 Dr. Shau Hamdan 5071
67 Dr. Cristogone Justine 4968
68 Dr. Conrade Ngonyani 4865
69 Dr. Deo B. Mwanakulya 4873
70 Dr. Lucy Laurent 4872
71 Dr. Khadija Juma 4969
72 Dr. Valentino Koja 5338
73 Dr. Aloyce F. Lengasia 4977
74 Dr. Zyleen Kasamali 4888
75 Dr. Mwajuma Mustapha 4971
76 Dr. Mariam Hamad 4859
77 Dr. Francis Mwimazi 4967
78 Dr. Hassan Barnabas 5364
79 Dr. Grace Mmasi 5045
80 Dr. Mohamed Mzige 4860
81 Dr. Elias Paschal 4961
82 Dr. Farida Mtonga 5002
83 Dr. Gabriel Mbwete 5337
84 Dr. Magdalena Dennis 4910
85 Dr. Ahmed Ahmed 4798
86 Dr. Joseph Shaban 5408
87 Dr. Prudence Premier 5409
88 Dr. Malaja Ng’wigulu 5019
89 Dr. Biswaro Malima 4975
90 Dr. Isaac Mlay 5007
91 Dr. Raymond Samwel 5017
92 Dr. Michael Kiremeji 5376
93 Dr. Viviene Mlawi 5000
94 Dr. John Jananga 5380
95 Dr. Said Ibrahim 5020
96 Dr. Alphonce Simbila 5047
97 Dr. Catherine Mlowe 5044
98 Dr. Barbara Mwaipola 4964
99 Dr. Joel J. James 5129
100 Dr. Bright Sangiwa 5053
101 Dr. Evance Alexander 4887
102 Dr. Martha Nkya 5335
103 Dr. Camilla Kinemo 5406
KCMC 
1 Dr. Malkiadi P. Mbota 5208
2 Dr. Wilfred j. Meza 4900
3 Dr. Shomari O. Masenga 4983
4 Dr. Jamila J. Shemweta 5009
5 Dr. Godbless E. Massawe 5026
6 Dr. Rahel T. Mwavika 4879
7 Dr. Eliakimu P. Kapyolo 5032
8 Dr. Godfrey N. Barabona 5051
9 Dr. Aristides K. Raphael 4984
11 Dr. Emmanuel M. Manyonyi 5077
12 Dr. Herielly O. Msuya 5118
14 Dr. Noel J. Makundi 5142
15 Dr. Maxigama Y. Ndosi 5107
16 Dr. Patrick A. Karua 5137
17 Dr. George C. Mgalega 5155
18 Dr. Juma Adinan Juma 5151
19 Dr. Kenneth J. Mlay 5158
20 Dr. Njengo B. Mbanga 5145
21 Dr. Yesige A. Mutajwaa 5171
22 Dr. Mbazi D. Shemwetta 5139
23 Dr. Mwanaidi S. Mkwizu 5141
24 Dr. Peter E. Ng’wamkai 5109
25 Dr. Tumaini D. Ndibwire 5131
26 Dr. Lucas D. Ngamtwa 5161
27 Dr. Goodluck J. Ulomi 5143
28 Dr. Juma M. Nahonyo 5150
29 Dr. Emmanuel S. Masatu 4899
30 Dr. Angela E. Pallangyo 5110
31 Dr. Casto E. Mlay 5182
32 Dr. Birjna A. Hirani 5152
33 Dr. Anette J. Kessy 5178
34 Dr. Ester P. Lazaro 5190
35 Dr. Mugisha N. Nkoronko 5115
36 Dr. Sofia A. Ottaru 5146
37 Dr. Raya Y. Mussa 5132
38 Dr. Regina Y. Msanga 5148
39 Dr. Delfina R. Msanga 5147
40 Dr. Allen G. Kangarawe 5138
41 Dr. Sia C. Kiwia 5198
42 Dr. Peter E. Kipiki 5144
43 Dr. Avelina R. Kimaryo 5177
44 Dr. Peter F. Mwandiga 5075
45 Dr. Daimon B. Mwasamila, 5210
46 Dr. Emmanuel D. Lema 5185
47 Dr. Karungi J. Karoma 5130
48 Dr. Fortunatus m. Ibreck 5199
49 Dr. Sadiq S. Dawood 5121
50 Dr. Witness M. Mchwampaka 5186
51 Dr. Azza A. Naif 5111
52 Dr. Malkiadi P. Mbota 5208
53 Dr. Mariam T. Johari 5013
54 Dr. Daniel M. Chochole 5162
55 Dr. Oliver T. Masoy 5197
56 Dr. Gerald C. Robi 4927
57 Dr. Erasto S. Odindo 5229
58 Dr. Kasirye J. Collins 5243
59 Dr. George D. Dilunga 5239
60 Dr. Emmanuel S. Maro 5240
61 Dr. Irene R. Haule 5242
62 Dr. Godfrey A. Kisuma 5246
63 Dr. Frank M. Sudai 5231
64 Dr. Annette A. Marandu 5196
65 Dr. Joseph E. Soka 
66 Dr. Hans Mpimilwa 
MBEYA REFFERAL 
1 Dr. Msafiri Lewanga 5069
2 Dr. Regan Rajuu 5224
3 Dr. Alex Mwakyandile 5311
4 Dr. Osmundi Dyegula 4954
5 Dr. Ireene Kato 5012
6 Dr. Lutaragula Masili 5067
7 Dr. Nindwa Maduhu 5209
8 Dr. Noel Dominic Swai 4952
9 Dr. Masanja Erasto Kasoga 5100
10 Dr. Mwanahamisi Japhary 4768
11 Dr. Nuru Mwambola 5100
12 Dr. Jane Maganga 5174
13 Dr. Karim Mohamed 4767
14 Dr. Joyce T. Massaro 5195
15 Dr. Kanjanja A. Amas 5213
16 Dr. Joseph Msemwa 5116
17 Dr. Jonas Lulandara 4851
18 Dr. Kulwa Itambula Joseph 5173
19 Dr. Josephat Mapunda 4890
20 Dr. Joseph Antony Legembo 5392
21 Dr. Saili Mbukwa 5381
22 Dr. Samwel Cherubini Mkumbe 5395
23 Dr. Serephine J. Mrosso 4950
24 Dr. Agapiti Hipoliti Chuwa 4903
25 Dr. Deusdedit Kalaso 4986
26 Dr. Ano A. Maseta 5437
27 Dr. Alinanuswe Kasililika 4953
28 Dr. Anicetus Rwebangira 5123
29 Dr. David Hamisi Mvunta 5172
30 Dr. Ally Mbwana Mhando 5327
31 Dr. Aminiel E. Ngomuo 5068
32 Dr. Emmanuel Obasy Mwakibinga 5010
33 Dr. Erica A. Balama 4687
34 Dr. Fred Frank 5281
35 Dr. Emmanuel Bahemana 5070
36 Dr. Elisonguo E. Kimambo 5282
37 Dr. Furaha Mwakafwila 5108
38 Dr. Emmanuel J. Itambu 4685
39 Dr. Beniedy A. Chitama 5205
40 Dr. Gwakisa John 5023
41 Dr. Charrido Chalo 
42 Dr. Winfrida Halinga 5435
43 Dr. Wistone I Ngaiza 5441
44 Dr. Honsia E. Moshi 5288
45 Dr. Lewanga Msafiri 5069
46 Dr. Peter Frank Saria 5202
47 Dr. Ngwilo Mwakyusa 5317
48 Dr. Adison Mpyambala 4955
49 Dr. Ilekizemba G. Khalfanis 4420
50 Dr. Angela T. Mlole 5013
51 Dr. Rajab Mramba 5245
52 Dr. Lusajo Raphael Mwakajoka 5441
53 Dr. Musa Gabriel 377
54 Dr. Bogias Fidelis Mwamgunda 378
55 Dr. Raymond Mwalonde 5230
BUGANDO MEDICAL CENTRE 
1 Dr. Lukansola Makubula 4863
2 Dr. Amos Stanley 4876
3 Dr. George B. Rweyemera 4913
4 Dr. Peter J. Kitenyi 4925
5 Dr. Florian Mutasingwa 4918
6 Dr. Mwanaisha Seugendo 4905
7 Dr. Derick David 4884
8 Dr. Baraka R. Mkinze 4883
9 Dr. Emanuel Alphonce 4911
10 Dr. Paulina M. Manyiri 4891
11 Dr. Wilhelmina J. Mbwana 4924
12 Dr. Jacqueline B. Iraba 4941
13 Dr. Dismas Stephen 4934
14 Dr. Deo Donald Kisaka 4989
14 Dr. James J. Gesimba 5008
16 Dr. Athuman M. Mambo 4988
17 Dr. Hadija M. Bushahu 5015
18 Dr. Cosmas H. Mbulwa 4942
19 Dr. Raymond M. Wilson 5041
20 Dr. Elizabeth N. Kwiyolecha 5065
21 Dr. Flavian Simula 5165
22 Dr. George Adriano 5035
23 Dr. Enock J. Simeon 5079
24 Dr. Devotha J. Mbabala 5153
25 Dr. Hellen Munaku 5135
26 Dr. Kilemo J. Mzobora 5192
27 Dr. Shija F. Mahenda 5164
28 Dr. Frank Mayaya 5136
29 Dr. John N. Akwitende 5223
30 Dr. Dorice L. Shangali 5193
31 Dr. Albert J. M. Mnyanzilu 364
32 Dr. Amina J. Yusuph 5102
33 Dr. Immaculate Henry 5188
34 Dr. Deus R. Luhanga 5258
35 Dr. Noreen Jandwa 5279
36 Dr. Flora Willy Rumoka 5299
37 Dr. Gabriel C. Makenga 5303
38 Dr. Joel L. Maduhu 5307
39 Dr. Joan J. Nguma 5298
40 Dr. Museveni N. Justine 5349
41 Dr. Emanuel Nhonoli 4847
42 Dr. Ally Akrabi Munir 4773
43 Dr. Regina Mtayangulwa 4753
AMANA 
1 Dr. Fredrick Tembo 5265
2 Dr. Daudi Hassan 5267
3 Dr. Tumaini Bryon 5247
4 Dr. Tenga Yerko 4886
5 Dr. Majala Maulidi 4870
6 Dr. Elice Mweluka 4877
7 Dr. Kibona Samwel 5296
8 Dr. Abdulrahan Amin 5037
9 Dr. Alexander Kailembo 366
10 Dr. Mwanaasha Malewenga 5448
11 Dr. Valeria Ndomba 5390
12 Dr. Anna Sanga 5016
13 Dr. Luoga Prospelia 4850
14 Dr. Georgia Kamese 5052
15 Dr. Ally Mbikilwa 5450
16 Dr. Peter Kyabaroti 5016
17 Dr. Mamelita Basike 5402
18 Dr. Mariam Msimbe 5191
19 Dr. Khadija Msami 5300
20 Dr. mosses Wamoa 5038
21 Dr. Jasinta Lugila 5363
22 Dr. hellen Machagge 5249
23 Dr. Anna Asenga 5265
24 Dr. Salum Mruma 5268
25 Dr. Neema Ntamanwa 5291
26 Dr. Fatuma Kibao 5316
TEMEKE 
1 Dr. Godbless Charles 5168
2 Dr. Henry Jason Tarimo 4632
3 Dr. Clephace G. Mtana 4907
4 Dr. Daniel Joseph Mganyizi 4992
5 Dr. Elisha Otieno Osati 5336
6 Dr. Tony Mitala Luwukya 5455
7 Dr. Emmanuel G. Badya 4912
8 Dr. Phillipo S. Muhochi 4993
9 Dr. Alen Oden Kitalu 4994
10 Dr. Frexon Liseki Kiandiko 5180
11 Dr. Rose Sikazwe 5214
12 Dr. Nevelin Hezron 5216
13 Dr. Daniel A. Mashamba 5212
14 Dr. Hadija M. Kimwaki 5260
15 Dr. Lucas James Maiga 5400
16 Dr. Odiwa C. Ombati 5452
17 Dr. Thomas D. Kapela 4906
ST. FRANCIS IFAKARA 
1 Dr. Greyson Mpinga 5403
2 Dr. Kasanzu Masanja 5262
3 Dr. Haitham Mohamed 5450
4 Dr. Massanja Dotto 5263
5 Dr. Nicholaus Sayana 4937
6 Dr. Kahibi Bernard 5055
7 Dr. Emmanuel Kimario 5098
8 Dr. Rebeca Majige 5064
9 Dr. Allen Kissanga 5321
10 Dr. James Zakaria 5326
11 Dr. Kurenje Mbura 5264
12 Dr. Nyambura Moremi 4920
13 Dr. Donald Kenedy 5056
14 Dr. Elipokea Sarakikya 5314
15 Dr. Magreth Kagashe 4894
16 Dr. John Mrina 4843
17 Dr. Sebastian Pima 5053
M/ NYAMALA 
1 Dr. Veronica Lyandala 4908
2 Dr. Goodluck Mlimbila 4938
3 Dr. Geofrey Seusi 4923
4 Dr. Zena Suleiman 5087
5 Dr. Fadhil Mlimbila 5225
6 Dr. Wilfred Rutahoile 4882
7 Dr. Ikupa Mwasubi 5076
8 Dr. Janeth Mandepu 5025
9 Dr. Paul Swakala, 4928
10 Dr. Mwandu Makani 4929
11 Dr. Vivian Rugarabamu 5033
12 Dr. Mufida Mshimba 5133
13 Dr. Didas Patris 5069
14 Dr. Adelina Rutashobya 5112
15 Dr. Kunge Klint 5235
16 Dr. Pius Ezekiel 5272
17 Dr. Daniel Hubert 5290
18 Dr. Petro Sewa 5271
19 Dr. Diana Damian 5331
20 Dr. Egbert Eslone 5340
21 Dr. Meshack Ole Sabaya 5432
22 Dr. Manyere J. Kapongo 5428
23 Dr. Joseph Mkenda 5429
24 Dr. Wendy Robert 5430
25 Dr. Eshmedi Mathayo 
26 Dr. Jualako Nassoro 4775
SEKOU TOURE HOSPITAL 
1 Dr. Akili Msei 5412
2 Dr. Patrick Mhagama 5415
3 Dr. Vitalis Ruyimba 5422
4 Dr. Robert Onesmo 5418
5 Dr. Catherine Moshi 5463
6 Dr. Musyangi Tekele 5445
7 Dr. George Ngimba 5420
8 Dr. Elias Ndongo 5275
9 Dr. Belkumas.H. Mbawala 5454
10 Dr. Ezekiel Kambona 4948
11 Dr. Zakayo Ilomo 5444
12 Dr. Yahaya Nasoro 4781
13 Dr. Rehema Mwabaya 5459
14 Dr. Grace Bash 5464
HYDOM HOSPITAL 
1 Dr. Edwad Lengai 4990
2 Rommy andrew 5389
3 David Mgaya 4854
4 Innocent mtenga 5049
5 Edward Joseph 5011
6 Israel Alexseko 4901
7 Angelo Joachim 5042
8 Deogratius Baruba 4991
9 Johnson Joachim 5034
10 Evarist Kentgen 5043
11 Gabriel M. Soko 4915
DODOMA REGIONAL HOSPITAL 
1 Gustavus Deusdedith 5385
2 Cassian G. Mkuwa 5384
Imetolewa na: 
Dkt Donan Mmbando
MWENYEKITI- BARAZA LA MADAKTARI TANGANYIKA
11 Julai, 2012.

MAMIA WAFA MAJI MEDITERRANEAN

Ni wahamiaji walikuwa wakikatiza bahari kuelekea nchini Italy

Monday 9 July 2012

ICE ROAD TRUCK


Malori kwenye njia za barafu.safari yenye mashaka safari yenye kila aina ya kufikirika kwani ndani ya safari hii.Magari makubwa yanayofanya kazi ya kusafirisha mizigo mizito toka kwenye makampuni tofauti haswa yale ya mafuta na gesi.Yanatumia njia hizi za mkato kwenye barafu iliyokomaa na sehemu nyengine isiyokomaa na kupelekea madereva kupata matatizo ya kila aina lakini kwa uzoefu wa madereva wa ICE ROAD TRUCK wanaweza kufanikiwa kwenda na kurudi wakiwa wameacha historia nzito
Sasa ICE ROAD TRUCK iko nchini India sehemu yenye njia mbaya isiyo na mfano,Milima mikubwa pamoja na ajali zilizo wacha baadhi ya magari yakiwa chuma chakavu..
Kaa nasi tukujuze yatakayo jili nchini India 

DEREVA KUWA MAKINI


Hizi ndio njia ngumu na kona mbaya haswa kipindi cha majira ya baridi...Oslo

Tuesday 3 July 2012

MAPACHA WAACHANA

Bendi ya mapacha watatu imekumbumbwa na mmemme nyeko baada ya múasisi mwenzao kuondoka..Chanzo chetu kina ng amua ya kwamba Kalala JR ameondoka Bendi ya mapacha watatu bila ya ugomvi wala mkwaluzo wowote..Imekuwa ni kawaida ya wanamuziki kuama toka bendi moja kwenda nyengine au kuanzisha bendi...Japo ni tabia ya kimaslai lakini Ngwamba letu linadadavua baadhi ya wanamuziki wanaohama bendi wengine urudi walipotoka na kuendeleza kuwakuna mashabiki wao kama kawaida

Saturday 23 June 2012

Mandhali ya mji wa Bwagamoyo 1860

Hii picha ilipigwa miaka 30 iliyopita.
Ahsante kwa Ngwamba letu aliopo kwenye likizo
Tunakutakia likizo njema na furahia mandhali ya mji huo

Mfalme ndani Juger

Lilikuwa speed camera yetu imeshindwa kumnasa vizuri

MADAKTARI ACHENI KAZI SERIKALINI

Kugoma sio dawa ya tatizo.Dawa ni kuacha kazi ya kutumwa na serikali na kuungana kuanzisha Hospitali yenu itakayokizi mahitaji na iliyo bora.

Wengi wenu ni madaktari bingwa kwa nini msiombe mikopo mikubwa na kujiajili wenyewe kwa kuanzisha hospital yenu na kujilipa mishahara mikubwa..

Mkiwa na hospitali yenu mtanunua vifaa vya kisasa na wananchi watakuja kwenu na hata hao wanaotibiwa nje ya nchi pia watavutiwa na huduma zenu ziliboreshwa vzr.

Rejeeni kazini na mjipange upya.kuweni na mikakati endelevu kama wenzenu wa nchi nyengine ..

Wajulisheni wananchi mmeacha kazi ili muanzishe hospitali yenu yenye kiwango mtakacho lizika nacho.

Kimtazamo hamuigomei serikali mnamgomea yule raia alie lala na kulalama kwa maumivu uku ndugu yake akimuangalia akiteseka hadi kumfia mkononi mwake wakiwa wanaangaliana hali ameishaiaga dunia..

WASHKAJI KIBAO NDANI YA DAR LIVE



Friday 22 June 2012

MAHAKAMA KUU YAPIGILIA MSUMALI MGOMO WA MADAKTARI

Kufuatia Tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza 
mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012,
 Mahakama Kuu ya Tanzania,Kitengo cha kazi,Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha 
Madaktari Tanzania (MAT) yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
·        Amri hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania 
(MAT).
Sababu za msingi amabazo zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri hiyo upande mmoja ni pamoja na;·       

*Iwapo mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa madhara yake ni makubwa isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza maisha n.k 
·         *
Wajibu maombi, ambao ni MAT, inaundwa na Madaktari ambao wapo katika Sekta ambayo inatoa huduma mahsusi (essential service sector),

Aidha Chama cha Madaktari Tanzania kimetangaza mgomo bila kufuatia taratibu zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha Sheria ya Kazi (Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004.Masharti hayo ni ·       

 *Kuzuia wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama wakigoma, ·        

*Kuwepo na makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi wakati mgomo ukiendelea. 

Kwa misingi hii, Mahakama Kuu ya Tanzania, kwa Chama cha Madktari Nchini, na wanachama wake, inaamuru kusitisha na kutoshiriki katika mgonmo huo.

UWEZI KUAMINI!APANDA KILIMANJARO KWA MIKONO