Wednesday, 19 September 2012

HALI YA HEWA IMEANZAA KUBADILIKA

Majira ya baridi ndio hayo kwa wanaoishu pande zile za kule muda ndio huu wa kulisogeza koti

Tuesday, 18 September 2012

BWAGAMOYO YAZIDI KUNG ALA



JK Aweka Jiwe La Msingi uzinduzi  Ujenzi Wa Barabara Ya Bagamoyo-Msata


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Msata uliofanyika katika kijiji cha Kiwangwa wilayani Bagamoyo leo mchana.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi, Kaimu Mkuu wa mkoa wa Pwani ambaye pia ni mkuu  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik(Wapili kushoto),Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli(wanne kushoto) na kulia ni Waziri wa Mazingira Mhe. Theresa Hoviza.

Ndoto ya miaka mingi ya kujengwa kwa barabara ya Msata-Bagamoyo kwa kiwango cha lami imetimia leo, Jumanne, Septemba 18, 2012, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipoweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara hiyo katika sherehe kubwa iliyofanyika eneo la Kiwangwa.
Barabara hiyo ya kilomita 64 inajengwa na mkandarasi wa ndani ya nchi, Estim Construction, na inagharimiwa asilimia mia na Serikali ya Tanzania bila msaada kutoka kwa mfadhili yoyote.Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania, Injinia Patrick L. Mfugale amesema kuwa barabara hiyo inayogharimu kiasi cha Sh. bilioni 94, ikiwa ni pamoja na fedha za fidia na kumlipa mkandarasi mshauri, itakamilika Juni mwakani.

Pamoja na kwamba Mheshimiwa Rais ameweka jiwe la msingi kwenye barabara hiyo, Injinia Mfugale amesema kuwa mkandarasi wa sasa alianza ujenzi tokea 2010 baada ya usanifu wa barabara hiyo kukamilika na baada ya Serikali kumtimua mkandarasi wa mwanzo wa barabara hiyo, TACOPA, Novemba 13, mwaka 2009.Amesema kuwa mpaka sasa barabara hiyo imekamilika kwa asilimia 65, yaani kwamba kiasi cha kilomita 36.7 tayari zimewekwa lami na kuwa ni kilomita 23 zilizosalia na ambazo zitamalizika katika miezi tisa ijayo.Injinia Mfugale amesema kuwa mpaka sasa Serikali imekwishakulipa kiasi cha Sh. bilioni 56.8 ikiwa ni pamoja na fedha iliyolipwa kama fidia kwa wananchi ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo.Amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo hautahusisha ujenzi wa daraja kwenye Mto Ruvu kwa sababu usanifu wa daraja hilo ulichelewa kidogo kukamilika hata kama tayari sasa umekamilishwa.

Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa John P. Magufuli amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ni sehemu ya ujenzi wa kilomita 11,154 za barabara za lami zinazojengwa na Serikali ya Mheshimiwa Kikwete.“Nataka muelewe vizuri maana ya kilomita hizi. Wakati wa Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, tulikuwa na barabara za lami zenye urefu wa kilomita 1,330. Kati ya Uhuru na mwaka 2005, tulijenga barabara zenye urefu wa kilomita 6,500 na kati ya 2005 na sasa tunajenga barabara zenye urefu wa kilomita 11,154,” amesema Waziri Magufuli.Waziri huyo amerudia msimamo wake kuwa kamwe Serikali haitawaachia watu wanaojenga ama kufanya shughuli katika eneo la hifadhi ya barabara bila kuwachukulia hatua.

Naye Rais Kikwete amewaambia mamia kwa mamia ya wananchi walioshiriki katika sherehe hizo kuwa barabara ndiyo mishipa ya damu ya uchumi wa nchi yoyote na ndiyo maana Serikali inatenga kiasi kikubwa katika Bajeti yake kwa ajili ya ujenzi wa barabara. Amesema kuwa katika Bajeti ya sasa, barabara zimetengewa kiasi cha Sh. trilioni 2.2 ambacho ni kiasi kikubwa cha pili baada ya Bajeti ya elimu.Rais Kikwete amesema kuwa pamoja na faida zake kubwa na nyingi, barabara hiyo itakuwa na changamoto zake ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa ajali za barabara, kuongeza urahisi wa kusambaa kwa ugonjwa wa ukimwi na hata kuvutia watu wenye lengo la kununua ardhi kubwa ya wanavijiji ambako inapita barabara hiyo.Rais pia ameungana na Waziri Magufuli kwa kuonya: “Kama alivyosema Waziri, wanaoifuata barabara watavunjiwa nyumba zao na hawatalipwa, lakini wale ambao barabara inawafuata watalipwa hata wakivunjiwa.”

Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu.Dar es Salaam. 18 Septemba, 2012

Thursday, 13 September 2012

Amuacha aliemsachi kwenye reli

Mannen lämnar perrongen - efter att ha rånat Jerry som ramlat ner på tunnelbanespåret.
Mtu anaetafutwa kwa udi na uvumba nchini sweden baada ya kumsachi na kuondoka na poketi uku traini kuja na kumkanyaga jamaa anaefahamika kwa jina la Jerry


Monday, 10 September 2012

STAZ 2 GAMBIA 1 NA GOZI Limekwisha


Mpira umekwisha na Tanzania 2 Gambia 1

Serena Williams ashinda US open

Tre stora tennistitlar på lika många månader är inte nog. Efter US Open-segern är Serena Williams fortfarande hungrig på fler titlar.

Ajisikia kijana mwenye njaa kwa ushindi wake,ameshinda Victoria Azarenka6-2,2-6,7-7

Thursday, 6 September 2012

UJENZI BAGAMOYO ROAD UNAVYOENDELEA

Ujenzi wa barabara ya Bagamoyo unazidi kusonga mbele na wenye matumaini makubwa licha ya foleni za hapa na pale lakini mambo mswano

ONYO PICHA HIZI ZA KUTISHA


TUKIO LA KUUWAWA DAUDI MWANGOSI AKIWA MIKONONI MWA WALINDA AMANI 2012 MJINI IRINGA


Picha hii ni kwa hisani ya mtandao.Bint akimuangalia baba yake Sheakh Aboud Rogo muhubiri wa dini ya kiislam mjini Mombasa Kenya aliepigwa risasi hivi karibuni haya ndio yaliojili Afrika mashariki...Tunaomba viongozi wetu kukemea haya mambo kwa nguvu zao zote

Tuesday, 4 September 2012

MICHAEL DUNCAN TUTAKUKUMBUKA

Michael Clarke Duncan in The Green Mile
Galasa maarufu la cinema Michael Clarke mwana wa Duncan amefariki dunia baada ya 

kuugua kwa muda miezi mitatu kitandani kwa kusumbuliwa na ugonjwa wa 

moyo.Amekufa jijini Los Angeles siku ya jtatu 

Hakika mashabiki wake watamkumbuka kwa umahili wake wa kucheza cinema

AFRICA HAKUNA NJIA YA MKATO UKUAJI WA MIJI NA MAKAZI

Umoja wa Mataifa umeweka bayana kuwa hakuna njia ya mkato ya kukabilina na changamoto za kukuwa kwa miji zaidi ya kuwa na sera madhubuti za kuboresha na kupanua miji. Mwanzoni mwa karne ya 20 ni 2% tu ya watu ilikuwa ikiishi mijini. Leo ni 50%.

Picha pembeni ni jiji la Dar es salaam kama ilivyo naswa na ngwamba letu

Zetu dua unyonge una mwisho wake


KURA YA MAONI

Ni halali Polisi kutumia nguvu kupita kiasi?


 
 
 
 

Lango la dhahabu lenye ulinzi wa chuma

Lango kuu la dhahabu kwenye bustan mwanana yenye mandhali kuvutia ndani ya himaya malkia Victoria wa Scundanavia

ETI TUME YA NINI NA WAHUSIKA HAWA HAPA?


Mambo haya mpaka lini?mbona orodha inazidi kuongezeka,Songea.Arusha.Morogolo.Iringa na kwengineko 

Leo tuko shamba

Kwa mapicha na manyuzi ya shambazz yatakuwepo kama dawa kama kawa