Saturday, 9 June 2012

NA HII NDIO ZIMBABWE YA JOGOO MUGABE

Mmoja kati ya wenye kusoma ananena yalio moyoni,
Ilikuwa saa mbili asubuhi majira ya kwa Jogoo almaarufu kama Kidume Mugabe alipokwenda kufungua kinywa akiwa na kitu cha ONE HUNDRED TRILLION DOLLARS.mpango mzima ulikuwa hivi!chai moja andazi mbili na chapati yenye jina maarufu kitaa kile yaani chapati gazeti kwa wale wenye macho makali laiti kama utanyanyua usawa wa sura yako unaweza kumuona alie mbele yako...
Kwa kuwa yeye ni mzoefu upande wa kujiweka sawa panapo kuchwa akaagiza na arage ili mambo yawe sawa bin sawiya na mchana upite wima kama daladala lililouza kituo,
Mambo yote hayakuwa kama yalivyotarajiwa na badala yake HUNDRED TRILLION Ilimalizika na msela ajashiba na mchana haukuwa wenye kushedelele 
Kumbuka na hii ndio Zimbabwe ukitaka kushiba rudi kwenu

No comments:

Post a Comment

Angalia unapoandika usije kuleta machafuko
na hali ya sinto fahamu